ARSENE WENGER "AMTONGOZA" AUBAMEYANG KWA AJILI YA KUZIBA NAFASI YA SANCHEZ

KOCHA Arsene Wenger ametupa ndoano kwa nyota wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang kama njia ya kutaka kupata mbadala wa Alex Sanchez ambaye ana kila dalili ya kutaka kuondoka katika viunga vya Emirates.

Habari zilizopatikana kutoka mitandao ya kimataifa zinasema kwamba Arsenal imepania kumalizana na mchezaji huyo raia wa Gabon katika kipindi cha usajili wa dirisha la kiangazi kwa kitita cha pauni mil 52.

Kocha wa washika bunduki hao, Wenger alihamisha akili yake kwa nyota huyo huku akiweka bayana kuwa hana sababu ya kumbembeleza Sanchez.

Sanchez amekuwa katika hali ya kutokuwa na furaha ndani ya kikosi cha Wenger na kuna taarifa kwamba anataka kuachana na Arsenal ifikapo dirisha la kiangazi.

Kutokana na hilo, sasa akili ya wenger ni kwa nyota huyo wa kimataifa wa Gabon ambaye amekuwa katika kiwango cha juu sana kwenye timu yake ya sasa nchini Ujerumani.


“Pierre-Emerick Aubameyang yuko kwenye kiwango cha juu kabisa na haitakuwa ajabu kumsajili. Unaweza kufananisha uwezo wake na wakati ule nilipomsajili Nwanko Kanu wa Nigeria au Emmanuel Adebayor wa Togo,” alisema Wenger akikaririwa na mtandao wa Express Sport.

No comments