AS ROMA YABARIKI KWA MASHARTI UHAMISHO WA MOHAMED SALAH KWENDA LIVERPOOL


MKURUGENZI wa Michezo wa AS Roma, Ramon Rodriguez Verdejo, maarufu zaidi kwa jina la Monchi amesema hawana kipingamizi juu ya uhamisho wa straika wao Mohamed Salah kwenda Liverpool, lakini hawatakubali dau la chini ya pauni milioni 35.

Taarifa kutoka Italia zinapasha kuwa klabu hiyo ya Anfield iko tayari kuweka mezani ofa isiyozidi pauni milioni 30.

"Kwa Salah kuina ofa kutoka klabu ya Uingereza (Liverpool) lakini bei itapangwa na Roma, sin a wanunuaji," Monchi aliuambia mkutano wa vyombo vya habari wakati wa utambulisho wa kocha mpya, Eusebio Di Francesco.

"Kama nilivyosema kabla, Roma si ‘supermarket’. Roma ni timu ambayo itaiwakilisha Italia michuano ya Ulaya. Tulimaliza nafasi ya pili katika Serie A na mipango yetu ni kubaki na kikosi kizuri iwezekanavyo, lakini wakati huohuo hakuna klabu isiyouza wachezaji."


La Gazzetta dello Sport limeripoti kuwa winga huyo raia wa Misri amekubali dili la Liverpool na amewaambia Roma kuwa anataka kuondoka.

No comments