AVEVA, KABURU MAMBO MAGUMU... sasa kutumikia mahabusu hadi Julai 13

JANA Alhamisi, Juni 29, 2017, rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange “Kaburu” walifikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es Salaam kusikiliza mashitaka yao.

Aveva na Kaburu wameshitakiwa kwa makosa matano ambayo kwa mujibu wa sheria yanawanyima dhamana, hivyo wamelazimika kwenda rumande hadi Juni 13 kesi yao itakapoendelea chini ya hakimu Victoria Nongwa.

Makosa matano wanayotuhumiwa nayo viongozi hao wa Simba ni; Machi 5, 2016 Aveva anatuhumiwa kughushi nyaraka za kudai Simba dola 300,000 za Kimarekani ambazo ni zaidi ya sh. Mil 600.

Pili, Machi, 16 zilitumika nyaraka za uongo kulilipa deni kupitia benki ya CRDB Azikiwe Branch. Tatu ni kula njama na kutakatisha fedha kinyume cha sheria, kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani.

Kosa la nne Evans Aveva anatuhumiwa kutakatisha fedha ambazo alizipokea kupitia benki ya Baclays tawi la Mikocheni na tano, Kaburu anatuhumiwa pia kumsaidia Aveva kutakatisha fedha dola za Kimarekani 300,000 kupitia benki ya Baclays tawi la Mikocheni.


Kwa mujibu wa sheria, makosa ya kutakatisha fedha hayana dhamana hivyo rais wa Simba, Aveva na makamu wake, Geoffrey Nyange “Kaburu” watakuwa rumande hadi Juni 13.

No comments