AZAM FC: HATUTOTUMIA TENA MAMILIONI KWENYE KUSAJILI, TUTAELEKEZA NGUVU KATIKA KUWAPANDISHA WACHEZAJI WETU VIJANA

KLABU ya Azam FC imetangaza kuja na mfumo mpya ambapo sasa itawekeza zaidi kwenye kuwapandisha wachezaji wao vijana badala ya kutumia mamilioni katika usajili.

Msemaji wa Azam FC, Jafar Idd aliongea na waandishi wa habari na kusema kuwa wameamua kuja na mfumo huo mpya ili kuhakisha wachezaji wao vijana wanapata nafasi kubwa katika timu kwa kuwapandisha kwa idadi kubwa zaidi.

“Azam FC sasa tunakuja na structure mpya ya kuangalia usajili, lakini si kwa maana ya kutumia mabilioni ya pesa kama tulivyokuwa tukifanya zamani,” alisema Idd.

“Tumeamua kuwapromoti zaidi wachezaji wetu vijana na tunaamini itatusaidia tukitazama mfano wa Mbao FC, bajeti ya Mbao ya mwaka mzima inaweza ikawa ni bajeti ya Simba au Yanga ya mwezi mmoja tu.”


“Lakini Mbao pamoja na bajeti yao ndogo, wameweza kupambana na hii ina maana kuwa Tanzania ina vipaji ambavyo kama vitatengenezwa vizuri vinaweza kupambana barabara,” alisema Idd.

No comments