AZAM FC YACHOKA KUFICHA UKWELI, YAAMUA KUANIKA "KUMMIMINA" SAAD KAWEMBA

HATIMAYE Azam FC wametangaza rasmi kuachana na aliyekuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Saad Kawemba na kumshukuru kwa kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi chote cha uongozi wake.

Akiongea na waandishi wa habari jana, msemaji wa Azam FC, Jafar Idd Maganga alisema kuwa, kuanzia sasa Abdul Mohammed ndie atakuwa kiongozi wa juu wa klabu hiyo ya wana lambalamba wa Chamazi, Dar es Salaam.

“Namtakia kila la kheri Kawemba na baada ya mkataba wake kumalizika katika klabu hii ya Azam tunatangaza kuwa cheo chake kimeondolewa na hakitakuwepo tena klabuni,” alisema Maganga.

“Abdul Mohammed ambaye alikuwa General Manager wa klabu sasa ndio anakuwa top wa klabu ya Azam FC, kwa maana ya utendaji wa shughuli za klabu yetu.”

“Nafasi hii ilikuwa inashikwa na Saad Kawemba akitumia cheo cha “CO” lakini yeye anaondoka na anakuja Abdul Mohammed ambaye ndio atakuwa mtendaji mkuu wa Azam na sasa klabu iko ndani ya mikono yake.”

“Amepewa jahazi hilo aendeshe klabu kwa maana ya yeye kama yeye kuangalia mifumo yake na kujua azam anaitoa hapa ataipeleka wapi, hasa kwavile ana taaluma ya uandishi wa habari.”


“Sisi wengine tunamtakia kila la kheri Abdul ambaye pia ana taaluma ya juu kabisa ya accountant pamoja na masomo ya utawala aliyosomea Uingereza ambaye uongozi wa Azam umekaa na kuamua kumpa majukumu ya mtendaji mkuu,” alisema.

No comments