AZAM FC YAWATUPIA "MAGUNIA" AME ALLY ZUNGU NA HAMIS VIARI NCHA

KLABU ya Azam imewafungulia milango wachezaji Ame Ally Zungu pamoja na Hamis Viari Ncha ambao mikataba yao imemalizika klabuni hapo.

Azam walimpeleka Zungu Simba kwa mkopo ili kupandisha kiwango chake ambapo baadae aliombwa na Kagera na sasa mkataba wake umemalizika ambapo atakuwa mchezaji huru.

Mchezaji mwingine ambaye Azam walikuwa nae na sasa wamesema hawataweza kuendelea nae kutokana na maoni ya kocha, ni Hamisi Viari Ncha ambaye alikuwa Azam FC kwa muda mrefu na kutoa mchango mkubwa kwa timu.

“Viari hadi mkataba wake unamalizika alikuwa alikuwa bado yuko azam Football Club, lakini kwa sasa hatutokuwa nae, tunamtakia kila la kheri na tunaukumbuka mchango wake,” amesema Idd ambaye ni msemaji wa Azam FC.


“Ila niseme tu kwamba zoezi hili la kuchukua wachezaji ambao mikataba yao imekwisha na kuwaruhusu kwenda klabu nyingine linaendelea na hii ni awamu ya kwanza kwa wale ambao tayari wameshakabidhiwa barua zao mkononi.” 

No comments