BAADA YA CONTE KUMWAGA MBOGA, DIEGO COSTA AMWAGA UGALI CHELSEA


Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Diego Costa amesema amefahamishwa na meneja wa klabu hiyo Antonio Conte kwamba hayupo tena katika mipango ya klabu hiyo.

Costa, 28, alifunga mabao 20 katika mechi 35 alizocheza Ligi Kuu ya England na kuwasaidia The Blues kushinda taji hilo msimu lakini sasa anaonekana hana thamani tena Stamford Bridge.

"Mimi ni mchezaji wa Chelsea, lakini hawanitaki huko," Costa amesema.

"Antonio Conte amenijulisha kupitia ujumbe wa simu kwamba siendelei Chelsea na mambo yako hivyo. Conte amesema hanitegemei msimu ujao."

"Uhusiano wangu na kocha huyo umekuwa mbaya msimu huu. Ni aibu, tayari nimesambaza ujumbe huo kwa watu wa Chelsea waamue”.

Costa ambaye ni mzaliwa wa Brazil lakini huchezea timu ya taifa ya Uhispania alijiunga na Chelsea kutoka Atletico Madrid kwa £32m mwaka 2014.

No comments