BAKAYOKO AMFANYA ANTONIO CONTE KUMPIGA BEI NEMANJA MATIC MAN UNITED

KAMA unadhani meneja wa Chelsea, Antonio Conte amekoma kwa kitendo chake cha kumfukuza katika timu hiyo Diego Costa kwa meseje ya simu tu, utakuwa umekosea.

Kuonyesha kwamba hajali kinachotokea ikiwa ni pamoja na kelele za mashabiki, Conte amekuja na kali nyingine baada ya kutangaza kwamba anamuuza kiungo Nemanja Matic.

Habari hizi zinaweza kuibua hisia nyingi, hasa ikizingatiwa kwamba Matic mwenye umri wa miaka 28 ni fundi hasa, lakini kibaya zaidi anamuuzia adui silaha kwani anataka kumuuza kwa Manchester United.

Lengo la Conte ni kwamba anataka kufanikisha usajili wa kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko mwenye umri wa miaka 22 ambaye anauzwa kwa thamani ya pauni mil 42.
“Kila jambo linakwenda kwa mipango yake. Tunamuuza mchezaji na kusajili mchezaji mwingine. Na haya sio makosa ndio mipango ya soka ilivyo,” amesema.

Amesema kwamba kila mtu anajua uwezo wa Bakayoko na kwamba kwa umri wake wa miaka 22 atakuwa na msaada zaidi kwa kikosi chake ukilinganisha na umri wa matic ambao kimsingi umekwenda sana.

Kocha huyo amesema kwamba anajua anaweza kulaumiwa sana kama alivyolaumiwa kwenye suala la Costa, lakini yeye kama mwalimu anajua nani anamfaa na yupi anatakiwa ampishe.


“Mimi ndie nakaa na wachezaji hawa, najua kila mmoja mwenendo wake, najua pia kila mmoja ana nafasi gani na yupi anatakiwa kuongeza maarifa. Nayafahamu pia mahitaji ya timu kwa wachezaji inaowataka. Naomba mashabiki wanielewe,” amesema.

No comments