Habari

BAYERN MUNICH WASEMA WANA KIKOSI IMARA KISICHOHITAJI USAJILI WA KUTISHA MSIMU HUU

on

KIGOGO wa Bundesliga na
mabingwa watetezi wa Ujerumani, Bayern Munich wamesema hawana haja ya kufanya
usajili wa kutisha kutokana na ukweli kuwa kikosi kiko kamili na kimetimia.
Mkurugenzi wa michezo wa klabu
hiyo kongwe alithibitisha taarifa za kutosajili katika usajili wa majira ya kiangazi.
“Hatuna tulichokipanga kuhusu
usajili mpaka sasa. Ni sawa na kusema hatuna haja ya kufanya hivyo labda
litokee lolote la dharura,” alisema Sammer.
“Tumemuuliza kocha wetu
kuhusiana na suala la kusajili akatuhakikishia kuwa hakuna haja ya kufanya
usajili mkubwa akiamini kuwa kikosi kipo imara kwa ajili ya msimu huu.”

“Ila tumempa fursa ya kuangalia
kama anaweza kufanya usajili katika muda muafaka, nae amejibu kuwa ataangalia
kama kuna haja ya kuongeza wawili ama watatu, ila amejiridhisha kuwa na kikosi
bora cha kutetea ubingwa kwa mara nyingine msimu huu,” alisema mkurugenzi huyo.
  

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *