BEN POL AENDELEA KUTETEA PICHA YAKE ILIYOZUA UTATA MITANDAONI

MWANAMUZIKI Ben Pol ameendelea kutetea picha yake aliyoituma kwenye mitandao ya kijamii na kuzua gumzo kwa mashabiki wake.

Rapa huyo alituma picha inayomuonyesha akiwa amefungwa kama kwenye kiti kama mtu aliyekosa uhuru baada ya kutekwa na watu wasiojulikana.

“Mimi ni msanii, unapoona nimefanya kitu hata kama kitatoa ishara ishara tofauti lakini kikifanikiwa kuwa gumzo, maana yake nimefanikiwa katika sanaa yangu,” alisema rapa huyo.

“Sikuwa na lengo baya la kushitua, najaribu kuonyesha ujio wa kazi yangu ambayo itakuwa na maudhui ya mtu aliyetekwa,” aliongeza.


Benpol aliyepata umaarufu mkubwa baada ya kuachia vibao vyake kadhaa, vikiwemo vya “Sofia”, “Maneno” na “Moyo Mashine”, aliweka wazi kuja na kazi mpya ambayo pia itteka hisia za mashabiki wake wa muziki.

No comments