BEN POL AKUBARI OMBI LA KUFUNGA NDOA NA EBITOKE

MWIMBAJI wa miondoko ya R&B, Ben Pol amepokea la mcheza Komedi, Ebitoke aliyetaka kufunga nae ndoa.

Ben Pol amepokea ombi hilo na kuposti picha akionyesha kuheshimu hisia za staa huyo wa Komedi.

Ebitoke aliweka wazi kuvutiwa na maumbile ya Benpol ambapo aliamua kufunguka kuwa yuko tayari kufunga ndoa nae ikiwa ataridhia.

“Ben Pol ni mtu mzuri kwa ukweli, nilivyokutana nae mwenyewe alifurahi sana kuniona mimi, hata nami nilifurahi pia,” alisema staa huyo.


“Mwanzo nilijua angenichukulia tofauti, lakini nilivyokutana nae alionyesha kufurahi,” alimaliza staa huyo.

No comments