BEN POL BEN POL ATOBOA SABABU YA KUCHELEWA KWA VIDEO YA WIMBO WAKE WA "TATU"

MSANII wa bongofleva, Ben Pol ameeleza kwanini hadi sasa video ya wimbo wake mpya “Tatu” aliomshirikisha Darasa haujatoka.

Mwimbaji huyo amekiambia kipindi cha “Show Time” cha Radio Free Africa kuwa hawakutaka kutoa video ya wimbo huo kipindi cha mfungo wa Ramadhani ingawa hadi sasa imeshakamilika.


“Video ya “Tatu” imeshaisha na tayari ninayo, video imeshashutiwa na nipo nayo hapa ndani zaidi ya wiki moja sasa, naiangalia naonyesha na watu, sema tu kwenye muda ndio tunaangalia tutoe lini kwa sababu hatukutaka kutoa katikati ya Ramadhani kwa hiyo mwishoni mwa mwezi huu itatoka,” amesema Ben Pol.

No comments