BENITEZ AMUONYA MOUSSA SISSOKO KUJIUNGA NA REAL MADRID

RAFA Benitez amemuonya straka Moussa Sissoko kuacha mpango wa kutaka kutua Real Madrid.

Sababu ya onyo hilo ni kile alichodai kuhofia kwenda kuua kiwango chake kwani ushindani wa namba ndani ya Real Madrid ni mkubwa.

Sissoko amekuwa katika rada za Real Madrid tangu kumalizika kwa michuano ya Euro 2016 iliyofanyika nchini Ufaransa.

Katika michuano hiyo, Sissoko alionyesha kiwango cha hali ya juu hivyo kuzivutia timu mbalimbali, ikiwemo Madrid.

Sissoko amekuwa akiwindwa na mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa dau la euro mil 40.

“Natambua Real wanataka kuja kwangu. Ninawasubiri, najua wananihitaji sana kwa sasa.”

“Lakini ninachoweza kuona ni kwamba ndani ya Madrid kuna ushindani mkubwa wa namba.”

“Unaweza ukafurahia kwenda kule leo, lakini kesho ukaanza kujutia uamuzi wako lakini itakuwa tayari umeshachelewa,” alisisitiza Benitez.


Hata hivyo, Benitez alithibitisha kuwa klabu yake ya Newcastle haitakubali kumuuza straika huyo chini ya dau la euro mil 40 kwani bado ana mkataba wa miaka miwili kamili.

No comments