BEYONCE WA JAY Z ADAIWA KUJIFUNGUA WATOTO MAPACHA

TAARIFA kutoka kwa watu wa karibu na familia ya staa wa muziki nchini Marekani, Beyonce Knowles, zinasema mrembo huyo tayari amejifungua kimyakimya watoto mapacha wawili.

Inadaiwa kwamba msanii huyo alipelekwa hospitali ya West LA tangu Jumanne wiki iliyopita na tayari amefanikiwa kupata watoto wawili ambao mmoja ni wa kiume na mwingine wa kike, lakini familia hiyo haijaweka wazi suala hilo.

Baadhi ya walinzi wa msanii huyo walionekana wakiwa wamebeba viti viwili vya kubebea watoto hao mapema baada ya Beyonce kufikishwa hospitalini.


Mashabiki wa msanii huyo wameanza kutoa pongezi zao kwa Beyonce na mume wake, Jay Z kwa kuongeza familia na kufikia watoto watatu.

No comments