BILA ROMAN ABRAMOVICH BASI ANTONIO CONTE ILIKUWA BYE BYE CHELSEA


KAMA si bilionea Roman Abramovich kuingilia kati, basi kulikuwa na uwezekano mkubwa kwa miamba ya Italia, Inter Milan kumng’oa kocha Antonio Conte kutoka Stamford Bridge.

Hayo yamefichuliwa na gazeti la Corriere dello Sport la Italia, liliripoti kuwa Inter Milan ilimshawishi Conte kwa ofa ya pauni milioni 106 ili awatose Chelsea kiangazi hiki.

Kwamba bilionea wa Kichina anayemiliki klabu hiyo ya Serie A, Jindong Zhang, alikuwa tayari kumpa kocha huyo mkataba wa miaka 10 wenye thamani ya pauni milioni 10.6 kwa msimu.

Inter pia inadaiwa ilimuhakikishia Conte kumuunga mkono kikamilifu katika soko la usajili kwa kununua wachezaji awatakao ili kuunda kikosi imara.

Gazeti hilo limedai kuwa Conte alipelekewa maombi mwezi Mei, lakini aliwatolea nje baada ya bilionea wa Chelsea, Roman Abramovich kuingilia kati na kuilazimu Inter kuangukia kwa Luciano Spalletti.

No comments