BORUSSIA DORTMUND YASEMA HAITAMUUZA AUBAMEYANG BAADA YA JULAI 26


BORUSSIA DORTMUND imemwambia straika wake Pierre-Emerick Aubameyang, 28, kwamba ataruhusiwa kuondoka kiangazi hiki, lakini pale tu itakapotolewa ofa inayokubalika kabla Julai 26, tarehe ambayo klabu itaanza kambi ya maandalizi ya msimu mpya huko Bad Ragaz, Switzerland.

Liverpool na Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazomtolea macho straika huyo wa kimataifa wa Gabon aliyeibuka mfungaji bora wa Bundesliga msimu uliomalizika akifunga mabao 31 katika mechi 32, ambaye dau lake limepangwa kuwa pauni milioni 61.6.


Kocha mpya Peter Bosz, sambamba na mwenyekiti Hans-Joachim Watzke na mkurugenzi wa soka Michael Zorc, walifikia uamuzi wa kumruhusu Aubameyang kuondoka baada ya mkutano wao wiki hii.

No comments