BOSSOU ASEMA ANASUBIRI "NENO" TU KUTOKA KWA VIONGOZI WA YANGA ILI AREJEE JANGWANI

BEKI wa kati, Vicent Bossou amesema kwamba yuko tayari kurejea kwenye kikosi cha Yanga ikiwa tu viongozi wa klabu hiyo watamwita na kukaa meza moja ya mazungumzo.

Bossou ambaye kwa hivi sasa yuko nchini Togo kwa ajili ya mapumziko mafupi, alisema kwamba mpaka sasa hajawasiliana na viongozi kuhusiana na suala lake la mkataba mpya lakini atakuwa tayari endapo ataitwa.

“Hakuna mawasiliano yoyote ambayo yamefanyika mpaka wakati huu, lakini klabu ya Yanga naipa kipaumbele zaidi na nipo tayari kurejea endapo nitaitwa wakati wowote kuanzia sasa,” alisema beki huyo.

“Nipo mapumziko hivi sasa baada ya kuisha kwa mzunguuko wa Ligi na hakuna timu ambayo nimefanya nayo mazungumzo kwa ajili ya kujiunga nayo,” aliongeza.


Beki huyo ni miongoni mwa wachezaji wa kimataifa ambao wamemaliza mikataba ndani ya klabu ya Yanga ambayo kwa hivi sasa inafanyia kazi maoni yaliyoachwa na kochaGeorge Lwandamina juu ya wachezaji inayowahitaji.

No comments