BUFFON AMPIGIA DEBE GIENLIN DONNARUMMA KUJIUNGA JUVENTUS

MLINDA mlango mkongwe, Gianluigi Buffoni ni kama amempigia upatu mwenzake wa AC Milan, Gienligi Donnarumma,  baada ya kuutaka uongozi wa timu yake ya Juventus kumsajili wakati nyota huyo akijiandaa kutundika glovuzi.

Buffoni atakuwa nje ya mkataba wa kuitumikia klabu hiyo mwishoni mwa msimu ujao na nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 anatajwa kuwa huenda akatundika vitendea kazi vyake hivyo baada ya kumalizika fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Russia.

Mlinda mlango huyo mkongwe anadaiwa pia amepania kumaliza kibarua chake kwa heshima baada ya kupoteza kwa mara ya tatu mechi ya fainali ya Ligi kuu ya mabingwa dhidi ya Real Madrid iliyopigwa hivi kalibuni mjini Cardiff nchini Wales.

 Hata hivyo pamoja na malengo yake hayo, Buffon anazikaribia changamoto hizo kutoka kwa walinda milango hao vijana, Donnarumma nawa Arsenal, Wojciech Szcz esny ambao wanausishwa kujiunga na mabingwa hao wa michuano ya Ligi kuu ya Italia, Serie.

“kwangu mimi naona chaguo badala,” mlinda mlango huyu wa Italia aliwaambia waandishi wa habari kabla ya mechi yao ya jana ya kufuzu michuano ya kombe la dunia dhidi ya Liechtestein.

Ni sawa mara zote naamini kwamba mtu sahihi ni yule anayefaamu juu ya kitu.

Na ni sawa kwa Juve kujialibu kumsajili mlinda mlango kama yeye na nimlinda mlango sahihi kwa timu yetu ya taifa na katika hilo Gigio Donnarumma ndiye anayefaha,” aliongeza yota huyo.

No comments