CHAMA CHA MCHEZO WA JUDO CHAOMBA WADHAMINI KUISAIDIA TIMU YAO YA TAIFA

CHAMA cha Judo Tanzania (JATA), kimeomba wadhamini na wadau waweze kujitokeza kuisaidia timu ya timu ya taifa ya mchezo huo inayojiandaa na mashindano ya dunia yatakayofanyika mwezi Agosti, mwaka huu.

Akizungumza na saluti5, Katibu mkuu wa JATA, Innocent Mally alisema kuwa kwa sasa chama hicho kinahitaji fedha kwa ajili ya kusafirisha nchi katika mashindano hayo.

Alisema kuwa lengo la chama ni kuhakisha Tanzania inashirikisha wachezaji wa kila uzito ili kuwahakikishia wanakwenda kufanya vizuri katika mashindano na kuleta medali pamoja na kupata fursa ya kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Mally alisema kuwa wadau ndio kiunganishi ambapo watacheza kuisaidia timu hiyo ya taifa kwenda kuipeperusha bendera ya Tanzania vyema katika mashindano hayo ya mwaka huu.

“Kwa sasa chama tupo kwenye mchakato wa kuzungumza na wadau na wafadhili ili waweze kutuunga mkono katika kutusapoti kuhakikisha maandalizi ya timu yetu yanafanyika na hatimaye kwenda kushiriki,” alisema Mally.

Katibu huyo alisema kuwa mchakato utakaofanyika baada ya kupata fedha ni mchujo wa wachezaji ambao watakwenda katika mashindano kwa mwaka huu katika uzito tofauti tofauti.


Alibainisha kuwa kwa sasa timu iliyochaguliwa inashiriki mazoezi kwa pamoja chini ya kocha mzawa na inaendelea vizuri na maandalizi ya kujipanga kuhakikisha inakwenda kuiwakilisha vyema nchi.

No comments