CHARLES MKWASA: TUKO BIZE NA MIKATABA YA WACHEZAJI WALIOMALIZA MUDA WAO

KATIBU Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa wapo kwenye kipindi cha kuhangaikia mikataba ya wachezaji wao, baada ya kuwepo na idadi ya wachezaji tisa waliomaliza mikataba yao ndani ya kikosi hicho.

Mkwasa alisema kuwa wao kama uongozi, kwa sasa wanasubiri ripoti ya kocha George Lwandamina ili kupitia mapendekezo atakayoweka.

“Hatutatoka nje ya ripoti ya kocha kwa sababu hatutaki kuonea mtu au kumpendelea mchezaji yeyote bali tutaheshimu mawazo yake,” alisema Mkwasa.

“Tunaomba utulivu kwa Wanayanga wakati huu, kila kitu kinaendelea kwa amani na kinachosubiriwa ni ripoti tu.”


“Ni kweli kuna idadi kubwa ya wachezaji waliomaliza mkataba, lakini mara baada ya kupata ripoti Kamati ya Usajili itaingia kazini kwa nguvu zote,” alisema Mkwasa.

No comments