Habari

CHEICK TIOTE KIUNGO WA ZAMANI WA NEWCASTLE AFARIKI DUNIA

on

Kiungo wa zamani wa Newcastle United Cheick Tiote amefariki ghafla akiwa na umri wa miaka 30.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alifariki muda mfupi baada ya kuzimia wakati wa mazoezi nchini China, msemaji wa mchezaji huyo amesema.
Mchezaji huyo aliyekaa miaka saba Newcastle na kuichezea mechi 138 za Ligi Kuu, alihamia klabu ya Beijing Enterprises mwezi Februari.
“Ni kwa huzuni kubwa ambapo ninathibitisha kwamba Cheick Tiote alifariki mapema leo baada ya kuzimia wakati wa mazoezi,” msemaji wake alisema.
“Hatuwezi kusema zaidi kwa sasa na tunaomba kwamba familia yake iheshimiwe kipindi hiki kigumu. Tunaomba maombi yenu.”
Tiote alizaliwa Ivory Coast na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika 2015. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *