Habari

CHELSEA WAMMEZEA MATE KIUNGO KINGSLEY COMAN WA BAYERN MUNICH

on

MABINGWA wa England, Chelsea
wanamwangalia kwa jicho la tatu kiungo wa Bayern Munich, Kingsley Coman na sasa
wanamwinda kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha primier cha msimu ujao.
Matajiri hao wa jiji la Londo
wametajwa katika vita ya kumwania kiungo huyo ambaye anawindwa pia na klabu
mbalimbali za barani Ulaya.
Daily Star limeripoti pia tarifa
za The Blue kuingia vitani kwa ajili ya Coman.
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte
amemuelezea kiungo huyo raia wa Ufaransa kama mchezaji anayeweza kupambana
katika kikosi cha msimu ujao, hivyo amemweka katika kurunzi la usajili ujao.
Alisema: “Lazima tujipange kwa
ajili ya kutetea taji la msimu ujao pamoja na kuhimili mikiki ya michuano ya
Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.”

“Hivyo mmoja wa wachezaji
ninaowaona wana nafasi ndani ya kikosi chetu ni huyo Kingsley Coman, ambaye ni
kijana mwenye faida nyingi katika idara ya kiungo, lakini ana uwezo wa kucheza
kama mlinzi wa kati,” alisema Conte.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *