CHRISTIAN BELLA KUTUMBUIZA NA FERRE GOLA JUNI 29 DSM …Julai 1 ni Escape One


Mfalme wa masauti Christian Bella atatumbuiza kwenye onyesho kubwa litakalofanyika jijini Dar es Salaam Juni 29 sambamba na nyota wa rumba barani Afrika, Ferre Gola.

Onyesho hilo la ki – V.I.P litafanyika ndani ya hoteli ya Serena ikiwa ni maalum kwaajili ya mkesha wa siku ya uhuru wa Congo (DRC).

Meneja wa Christian Bella,  King Dodoo ameithibitishia Saluti5 juu ya onyesho hilo na kuongeza kuwa wawili hao watafanya onyesho lingine Julai 1.


Dodoo amesema onyesho la Julai 1 litafanyika ndani ya ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam.

No comments