CLAUDIO BRAVO NJIAPANDA MANCHESTER CITY

MLINDA mlango wa Manchester City, Claudio Bravo bado hajajua hatma yake ndani ya klabu hiyo, hivyo ni sawa na kusema yuko njiapanda.

Hilo linatokana na hatua ya kocha wake Pep Guardiola kutomweleza lolote juu ya kuendelea ama la, hasa katika kipindi hiki cha tetesi za usajili wa majira ya kiangazi.
Hii ni kwa mujibu wa Sky Sports.

Taarifa za mtandao wa klabu ya Manchester City zinasema kuwa Bravo bado hajaketi mezani na kuzungumzia kandarasi yake hata katika kipindi hiki.

Bravo aliyetua Man City akitokea Barcelona, ameshindwa kuonyesha kiwango cha kumshawishi kocha wake huyo ambaye hakuwa na msimu mzuri tangu achukue nafasi ya Joe Hart.

Bosi wa City, Pep Guardiola amenukuliwa akisema kuwa anahitaji kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kusuka kikosi cha msimu ujao wa premier. 

Kisha akaweka bayana namna asivyoridhishwa na uwajibikaji wa Bravo, hivyo kukosa imani ya kuamua kama atabaki nae kwa ajili ya msimu ujao ama la.


Bravo ameitumikia Barcelona katika michezo 73 tangu ajiunge nayo mwaka 2014 kwa dau la euro mil 12 akitokea Real Sociedad na kabla ya kujiunga na Manchester City.

No comments