CONTE AGOMA KUMTOA MARCOS ALONSO KWA DAU LOLOTE

PAMOJA na kuwepo kwa taarifa zinazomuhusisha kiungo wa Chelsea, Marcos Alonso kutakiwa na timu mbalimbali, lakini kocha Antonio Conte amekaririwa akisema hawezi kuuzwa katika klabu yoyote na kwa dau lolote.

Akinukuliwa, Conte amemwambia kiungo huyo raia wa Hispania kuwa bado yumo katika malengo yake ya misimu miwili ijayo, hivyo hawezi kuruhusu aondoke katika kikosi cha Stanford Bridge.

“Alonso ni kati ya wachezaji niliowaweka katika malengo ya muda mrefu, hawezi kuondoka hapa kwani ana kila sababu ya kuwemo katika kikosi cha misimu mingi ijayo.”

“Huwezi ukawa na kikosi imara pasipokuwa na wachezaji wazoefu kama yeye (Alonso), hivyo sipo tayari kukubali ofa ya aina yoyote kwa sasa.”

“Yumo katika mipango yangu ya kuimarisha kikosi cha msimu huu.”

“Ninachoshukuru ni kwamba ni mmoja wa wachezaji walio na uzoefu mkubwa wa Ligi, ni msaada mkubwa.”


“Ninampa nafasi katika mechi kadhaa za kuibeba timu na ninaamini ana uwezo wa kuonyesha kiwango chake cha misimu miwili iliyopita,” alisisitiza Conte.

No comments