CONTE AKIRI KUCHEMKA KUMFUKUZIA ROMELU LUKAKU

BOSI wa kikosi cha matajiri wa darajani, Antonio Conte amekiri kushindwa kuendelea kumfukuzia Romelu Lukaku anayekipiga katika klabu ya Everton, huku akitoa mojawapo ya sababu ya kushindwa kwake.     

Akizungumzia sababu hiyo, Conte aliweka bayana azma yake ya kutaka kumwamini straika wake mahiri Diego Costa.

Akinukuliwa kocha huyo aliyewapa taji la ubingwa wa primier klabu ya Chelsea alisema Costa na Lukaku ni kama wanafanana katika uwajibikaji, hivyo ameamua kuendelea kumwamini ndani ya kikosi kijacho.

“Nilikuwa katika mawindo ya muda mrefu kwa Lukaku, lakini nimeamua kuachana nae kwa sababu nina jambo la kuliweka sawa kwa Costa.”

“Costa ni kati ya washambuliaji waliochangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha azma ya kutwaa ubingwa wa premier msimu huu hivyo ni vyema nikaachana na Lukaku katika mbio za kumwania.”

“Nimekuwa nikimfuatilia kwa makini Diego na sasa nimejiaminisha kuwa ni mchezaji wa kiwango cha juu. Ni chaguo langu katika safu ya ushambuliaji.”


“Kusema ukweli Lukaku ni kati ya wachezaji wa kiwango kikubwa na kila timu inaweza kutamani kuwa nae, lakini nimeshindwa kumshawishi na akili zangu ninazibakiza kwa Diego,” alisisitiza Conte.

No comments