DAMIAN MARLEY ACHOMOA KUPIGA "SELFIE" NA SHABIKI WAKE WA KIKE

STAA wa muziki ya Reggae, Damian Marley ambaye alikuwa kwenye ziara ya muziki nchini Kenya, amefanya shoo na kuacha gumzo kutokana na kituko alichokifanya.

Damian amepanga kuzunguuka kwenye baadhi ya nchi za Afrika akifanya matamasha na tayari ameshatembelea nchini Kenya na kufanya shoo.

Moja ya vitu vilivyoshangaza ni kitendo chake cha kumpotezea dada aliyetaka kupiga nae picha kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata.


Kitendo cha Damian kinataka kufanana na kile alichokifanya Chris Brown alipofika Kenya kufanya shoo ambapo nae alidengua kupiga picha na mwanamke.

No comments