DARASA, ROMA, SNURA, BLUE NA ZANZIBAR STARS DAR LIVE IDD MOSSI

SIKU ya Idd Mosi Dar Live, Mbagala Zakheem inatarajiwa kuwaka moto kuanzia majira ya saa nne asubuhi ambapo kutakuwa na michezo mbalimbali ya watoto ikiwemo kuogelea na sarakasi.

Mtonyo mdogo tu wa buku tatu mlangoni unaweza kupenya ndani na kushuhudia burudani kutoka kwa msanii mkongwe wa Komedi, Bambo pamoja na makhirikhiri wa Tanzania waliojipanga vilivyo kwa ajili ya kukonga nafsi za watakaohudhuria.

Ile mida ya watu wazima itakapotimu, wasanii wakali wanaotikisa Bongo, kama vile Mr Blue, Stamina, Snura, Roma Mkatoliki, Darasa pamoja na bendi ya mipasho iliyoibuka upya ya Zanzibar Stars Modern Taarab, itakuwa ndo wakati wake.

Hiyo itakuwa ni kuanzia majira ya saa 2:00 usiku ambapo ukipenda kufaidi raha zote hizo utaombwa kuchangia kamchango kadoogo tu ka sh. 7,000 mlangoni na kuingia kula raha za kukata na shoka.


Taarifa kutoka ndani ya Dar Live zinasherehesha kuwa, kama ilivyo mila na utamaduni wa wa ukumbi huo, ulinzi wa raia na mali zao utazingatiwa kikamilifu huku pia parking ya magari ikiwa chini ya uangalizi mkubwa siku hiyo.

No comments