DAVID SILVA ASEMA ATATUNDIKA DARUGA BAADA YA KUTWAA KOMBE LA UEFA

STAA wa Manchester City, David Silva amesema kuwa ataweza kuachana na soka endapo atafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa akiwa na klabu hiyo ya jijini Manchester.

Staa huyo licha ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, Kombe la FA, wa Ulaya na Kombe la dunia, lakini bado hajawahi kuigusa tuzo hiyo kubwa kwa klabu za Ulaya.

Akizungumza na gazeti la Daily Mail akiwa kwenye mapumziko katika visiwa Canari vilivyopo pwani ya kaskazini mwa Afrika, staa huyo wa timu ya taifa ya Hispania alisema kuwa endapo atafanikiwa kutwaa ubingwa huo atakuwa amemaliza mataji yote anayotaka kuyabeba.

Msimu uliopita Man City ilitolewa hatua ya 16 bora kwa faida ya bao la ugenini baada ya kufungana kwa mabao 6-6 na timu iliyotinga hatua ya nusu fainali AS Monaco.

“Naweza nikastaafu,” alisema staa huyo.

“Endapo nitafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hapo naweza nikastaafu, kitakuwa ni kitu maalum kwangu,” aliongeza.

No comments