DEUS KASEKE KUONGEZA KANDARASI YA MIAKA MIWILI YANGA

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Deus Kaseke anatarajia kuongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo iliyobeba ubingwa wa Ligi Kuu bara kwa mara tatu mfululizo.
Kaseke aliyekuwa likizo kwao Mbeya, alirejea Dar es Salaam kuja kumalizana na uongozi wa Yanga baada ya kuwekewa mezani mkataba wa miaka miwili.
“Hakuna sehemu yoyote nitakayosaini zaidi ya Yanga ambao nimemalizana nao katika kila kitu muhimu,” alisema kiungo huyo.
“Yanga ni nyumbani, hizo taarifa za mimi kujiunga na Singida United nazisikia tu lakini ukweli ni kuwa ninasaini Yanga,” aliongeza.
Dues Kaseke amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha George Lwandamina tangu alipotua akitokea timu ya Mbeya City.

No comments