DIAMOND PLATNUMZ APIGA MARUFUKU TIFFAH DANGOTE KUJITUMBUKIZA KWENYE MUZIKI AKIHOFIA KUTONGOZWA

MSANII Diamond Platnumz amesema kuwa hatokubali mwanawe wa kwanza wa kike, Tiffah Dangote kujiingiza kwenye masuala ya muziki, kitu ambacho kinaweza kusababisha awindwe na wanaume kila kona.

Mwanamuziki huyo alidai kuwa yuko tayari kuunga mkono mtoto wa kiume kufanya kazi ya sanaa lakini sio kwa binti yake Tiffah

“Mwanamke anatongozwa kila pembe ya dunia na hasa unapokuwa msanii ni lazima uzongwe na kundi kubwa la wanaume, nisingependa hili litokee kwa binti yangu,” alisema Diamond.


Diamond alimpata mtoto huyo baada ya kuzaa mfanyabiashara maarufu wa Uganda, Zari ambaye hivi sasa anaishi nae kama mke na mume.

No comments