DIAMOND PLATNUMZ ASEMA KAZI MOJAWAPO YA WCB NI KUWAINUA WASANII KIUCHUMI

RAPA Diamond Plutnumz amesema kuwa moja ya kazi kubwa zinazofanywa na WCB ni kuhakikisha inamtoa msanii kutoka kwenye maisha duni na kumuinua kiuchumi.

Diamond alisema kuwa huwa wanahakikisha wanasaidiana wao kwa wao ndani ya kampuni ili kuhakikisha hawatofautiani sana kimaisha.

“Sisi ni vijana ambao tumeamua kujiajiri wenyewe kupitia muziki, hata kama haujawahi kulipa sana kwenye soko la Tanzania lakini bado wajibu wetu wa kubebana uko palepale,” alisema Diamond.

“Tunajua ugumu wa maisha ulioko mitaani ndio maana memba mpya anapopatikana lazima tuhakikishe kwanza anainuka kiuchumi, hii imesaidia kutuletea heshima,” aliongeza rapa huyo.


WCB ni lebo ya muziki ambayo ipo chini ya rapa Diamond Platnumz ambaye anatajwa kuwa msanii anayeingiza pato kubwa kuliko wote hapa nchini

No comments