DIDA AISHUKURU YANGA KWA KUMPA MAFANIKIO MAKUBWA KISOKA

KIPA anayetarajia kumaliza mkataba wake Juni 30, mwaka huu ndani ya yanga, Deogratius Munishi “Dida” amesema kuwa anaishukuru klabu hiyo kwa kipindi chote ambacho amekaa na kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi.

Dida ambaye hivi sasa akili yake imehamia Misri anakopanga kwenda kucheza soka la kulipwa, alisema klabu hiyo ndio iliyompa jina na kumjenga kimaisha.

“Mpango wangu wa kucheza soka la kulipwa nchini Misri hautokani na sababu za kutaka kuikomoa timu yangu ya Yanga kama inavyodhaniwa na watu, bali najaribu kutaka kutazama mbele zaidi,” alisema Dida.

“Maisha yangu kwa kiasi kikubwa yametokana na mchango wa Yanga, hivyo kamwe siwezi kubeza jitihada za klabu kunifikisha hapa nilipo,” aliongeza kipa huyo.

“Naomba ifahamike kuwa Yanga ndio klabu ninayoipa kipaumbele, hata nikienda mbali kiasi gani nitakaporejea chaguo langu ni Jangwani.”    


Ndoa ya Dida na Yanga itafika tamati mwisho wa nmwezi huu, huku yeye mwenyewe akisisitiza kutaka kwenda kucheza soka nje ya nchi.

No comments