DIEGO COSTA ASEMA: "NAONDOKA KIROHO SAFI CHELSEA, ILA NAJUA MTANIMISS TU"

MCHEZAJI nyota ambaye ametupiwa virago katika kikosi cha mabingwa wapya wa England, timu ya Chelsea, Diego Costa amesema kwamba anaondoka kiroho safi kabisa katika kikosi hicho.

Hata hivyo amesema kwa namna ambavyo kocha wake Antonio Conte amememfanyia kwa kumuondoa kibabe katika kikosi hicho, kuna siku atamkumbuka.

Conte amemwambia Diego kwamba hana mipango nae katika msimu ujao wa Ligi Kuu wa 2017/18 kwa ujumbe wa simu tu na mchezaji huyo amesema haina shida.

“Naondoka lakini nadhani kuna siku watanikumbuka, watajua kwamba kuna mtu aliyekuwa muhimu na mwenye maamuzi wakati wanapata shida,” alisema.

Costa amesema kwamba anaondoka katika klabu hiyo akiwa na amani kabisa na anakokwenda atapigania namba kuwa katika ubora wake uleule.

“Mimi ni Costa yuleyule, watu wanalalamika kwamba kwa nini nimeachwa lakini hayo ni maamuzi ya kocha, ameona sina nafasi kwake nami sina budi kuheshimu maamuzi yake. Naondoka kwa amani kabisa,” amesema.

Hata hivyo, amesema kwamba wakati wote atawaheshimu sana viongozi na mashabiki wa Chelsea kwani ameishi nao kama ndugu zake.


“Huwezi kujua, kuna siku naweza kurejea Chelsea, siwezi kuwachukia wote. Hata kocha naweza kukutana nae mahali kwingine,” amesema Costa.

No comments