DRFA YAANZA MIKAKATI YA KUANDAA KALENDA YA VIKAO, MATUKIO NA MASHINDANO

CHAMA cha soka mkoani Dar es Salaam (DRFA), kimeanza mikakati ya kuandaa kalenda ya vikao, mashindano na matukio mbalimbali ya chama hicho kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi ulioko madarakani.

Akiongea na saluti5, Katibu mkuu wa chama hicho, Msanifu Kondo alisema kutokana na kuepuka na usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara, wameamua kutengeneza kalenda hiyo ambayo itawasaidia kutambua mapema majukumu yao.

“Kalenda tutakayotengeneza tutaweka kila kila kitu wazi, lengo likiwa ni kila kiongozi wa chama kutambua majukumu yake na kuepuka migongano ya mara kwa mara,” alisema Kondo.


Alisema, kalenda hiyo itasaidia mambo mbalimbali ya chama kufanyika kwa wakati maalum na kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi wa chama hicho.

No comments