FABINHO WA MONACO BADO ANATAKA KWENDA MANCHESTER UNITED


KIUNGO wa Monaco, Fabinho ana nia ya kuachana na klabu hiyo kiangazi hiki na kwa mujibu wa gazeti la O Jogo, ameifanya Manchester United kuwa chaguo lake la kwanza mbele ya Manchester City katika usajili wa kiangazi hiki.

Raia huyo wa Brazil mwenye miaka 23, aliyekuwa sehemu muhimu katika msimu wa mafanikio Monaco, wakiipiku Paris Saint-Germain katika ubingwa wa Ligue 1, huku wakifika pia nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Old Trafford kutoka Stade Louis II.

Lakini Jumanne wiki hii, ripoti zilidai kuwa United wameamua kuachana na mpango wa kumfukuzia Fabinho na badala yake wanachunguza uwezekano wa kumsainisha Nemanja Matic kutoka Chelsea.

Kwa upande wake, mtandao wa ESPN FC umeripoti kuwa Jose Mourinho ameamua kumpotezea Fabinho kwa sababu anamtaka kiungo wa Tottenham, Eric Dier.

Taarifa za mwezi uliopita zilidai kuwa Manchester City chini ya Pep Guardiola ilikuwa karibu kukamilisha dili kwa Fabinho aliyeanzia beki ya kulia Monaco kabla kocha Leonardo Jardim kumhamishia kiungo cha ulinzi.

No comments