Habari

GARETH BALE AFUNGUKA KUHUSU KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED

on

Gareth Bale  ameweka wazi juu ya hatma yake, hususan kuhusu tetesi za uhamisho wake kutoka Real Madrid na kurejea  Premier League kiangazi hiki.
Ndani ya nyumbani kwao Cardiff, Jumamosi usiku Bale akatwaa taji la Champions League kwa mara ya tatu ndani ya misimu minne akiwa na Real Madrid baada ya klabu yake kuinyuka Juventus 4-1. 
Baada ya mchezo huo kocha Zinedine Zidane alikataa kujihakikishia uwepo wa Bale msimu ujao na kusema hilo litajulikana baadae.
Bale anahusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United, lakini mshambuliaji huyo wa zamani Tottenham alipoulizwa juu ya hilo alisema: “Nina furaha Real Madrid, tunashinda mataji na nina furaha kuwa hapa.”
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 alipoulizwa kama bado ataendelea kuitumikia klabu hiyo aliyojiunga nayo mwaka 2013, akasema: “Ndiyo. Nimesaini mkataba wa muda mrefu Real Madrid. Familia yangu ina furaha na nina furaha, hivyo tutendelea na kile tunachokifanya”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *