GARETH BALE SASA YADHIHIRIKA KUBAKI REAL MADRID KWA MUDA MREFU ZAIDI

SASA ni dhahiri kuwa kiungo wa Real Madrid, Gareth Bale ni kama vile amepigwa pingu na kwamba kauli ya sasa ya ndani ya klabu yake hiyo imebainisha kuwa hawezi kuondoka katika miaka ya hivi karibuni.

Hii ni baada ya kuwepo kwa mazungumzo mapya ya kutaka awe mchezaji wa kudumu, licha ya kandarasi yake ya sasa kuonyesha itafikia tamati ifikapo mwaka 2022.

Winga huyo raia wa Wales sasa amejifunga pingu kwa miaka sita hadi mwishoni mwa mwaka 2022, lakini kocha wake Zinedine Zidane ameomba Bale awe na mkataba mrefu zaidi ikiwezekana hadi mwaka 2026.

Bale mwenye umri wa miaka 28, alitua Real Madrid mwaka 2013 akitokea Tottenham Hotspur kwa dau lililovunja rekodi wakati huo la pauni mil 86.


Taarifa za ndani ya klabu hiyo ya jiji la Madrid zimebainisha kuwepo kwa mazungumzo yanayoendelea hivi sasa ya kutaka kiungo huyo amalize maisha yake ya soka ndani ya Madrid.

No comments