GENEVIEVE NNAJI AIPIGIA CHAPUO FILAMU YAKE MPYA YA "LION HEART"

GENEVIEVE Nnaji ambaye yuko mbioni kutoa filamu yake nyingine ya “Lion Heart”, amesema kuwa itakuwa na utofauti mkubwa ukilinganisha na nyingine zote alizowahi kucheza.

Filamu ya “Lion Heart” ipo chini ya uisimamizi wake wa moja kwa moja akiwa kama “Director” kazi ambayo ni mara yake ya kwanza kuifanya.

“Nimecheza filamu nyingi kama “The Wedding Part” na “Three Wise Men” lakini hii ya sasa naona ina utofauti mkubwa, inaonyesha ukomavu wa hali ya juu labda kwa sababu ipo chini ya usimamizi wangu wa moja kwa moja,” alisema staa huyo.


Katika filamu ya sasa, staa huyo amewatumnia wasanii wachanga kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyozoeleka.

No comments