GRIEZMANN AUCHANA UONGOZI WA ATLETICO MADRID AKISEMA ANATAKA KUSEPA ZAKE MAJIRA YA JOTO

MSHAMBULIAJI Antoine Griezmann ameuambia uongozi wa Atletico Madrid kuwa anataka kuondoka majira ya joto baada ya kuchoshwa na maisha ya Hispania.

Manchester United wamekuwa kwenye harakati za kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa na huenda akatua kwenye kikosi hicho cha kocha Jose Mourinho msimu ujao.


Griezmann amekuwa akiuliza mara kwa mara taaifa za Manchester United kupitia kwa rafiki yake mkubwa, Paul Pogba.

No comments