GUARDIOLA ASAKA SAINI YA BEKI WA GENOA YA HISPANIA

KATIKA mazingira ya kuendelea kukisuka kikosi chake, bosi wa matajiri wa jiji la Manchester, Pep Guardiola ameanza kupanga safu ya usajili wa dirisha la kiangazi kwa kusaka saini ya beki wa kati wa timu ya Genoa ya Hispania, Nicolas Burdisso.

City imekuwa katika mbio za kumsainisha nyota huyo kwa dau la pauni mil 22.

Hatua ya City kutaka kumwita kundini mlinzi huyo, ni kutokana na mkakati wake wa kuendelea kusuka kikosi imara cha kupigania hadhi na heshima.

Akinukuliwa, Pep alisema: “Nicolas Burdisso ni kati ya wachezaji muhimu kwa sasa walio katika kiwango cha juu, ana kipaji cha kuweza kucheza katika klabu yoyote kubwa, hivyo City haipaswi kumwacha.”

“Ana sifa moja kubwa, nayo ni kuwakabili washambuliaji wa timu pinzani na anajua kujipanga, hasa katika mazingira magumu.”

“Kingine ambacho ni sifa ya ziada ni kwamba ni mzuri katika kupanga safu ya ulinzi, hivyo ni mtu muhimu kwa sasa katika kiwango cha soka la dunia,” alizungumza Pep na kunukuliwa na The Goal.

“Sikuwahi kumshawishi kwa kiasi kikubwa lakini ninatambua uwezo alionao ambao ni muhimu kwetu. Kama klabu tutafanya jitihada za kumpata ili kuimarisha safu yetu ya ulinzi.”

“Kama atafanikiwa kutua kwetu nitajisikia furaha ya kupitiliza kwa sababu ndoto ya fikra zangu itakuwa imetimia.”

No comments