Habari

HAMIS KIIZA AWAPA YANGA KIUNGO KUTOKA UGANDA

on

YANGA iko katika mazungumzo
mengine na kiungo mmoja raia wa Uganda, Tony Maweje lakini kumbe usajili huo
unafanyika kwa ushauri wa aliyekuwa mshambuliaji wao, Hamis Kiiza “Diego”
aliyewapa sifa za mchezaji huyo.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga
ni kwamba Kiiza amewavuta Yanga na kuwaambia kuwa Maweje ndio mtu sahihi kwao
na kwamba endapo watampata watakuwa wamelamba dume kutokana na kazi yake.
Maweje mwenye uwezo wa kucheza
nafasi tatu uwanjani anajulikana kwa uwezo wake mkubwa katika kufanya majukumu
ya kiungo mkabaji na hatari mchezeshaji akiwa na uwezo mkubwa pia katika kupiga
mashuti makali na kufunga.
Mabosi wa Yanga wako katika
hatua za mwisho kutokana na taarifa za kukubali kila kitu katika uwezo wa
kiungo huyo ambaye atatua Yanga akitokea klabu ya Prottur FC.
Tayari kiungo huyo amekubali
kutua Yanga ambapo kwa sasa anajipanga kwa safari ya kuja kuitumikia Yanga
baada ya kukubaliana karibu kila kitu kuhusu uhamisho huo.

“Yanga tutamsajili huyo Maweje,
ni kiungo mzuri sana ambaye anajua kufanya kazi yake vyema, tumepewa ushauri
huo na Kiiza lakini hata tulivyomfuatilia pia tumemkubali, kiukweli anajua
kufanya kazi,” alisema bosi huyo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *