HARMONIZE ASEMA AKIONDOKA WCB ATAPASULIA NJE YA NCHI KWENYE LEBO KUBWA ZAIDI

MSANII wa bongofleva, Harmonize amesema kuwa ikiwa ataamua kujiondoa kwenye lebo ya Wasafi atajiunga na lebo nyingine kubwa zaidi kama “Young Money” na “Roc Nation”.

Harmonize amesema kuwa WCB ni moja kati ya lebo zinazofanya vizuri Afrika, hivyo hawezi kutoka kwenye lebo hiyo na kwenda kwenye kampuni nyingine za ndani.

“Nawezaji kuiacha WCB na kujiunga na kampuni nyingine ya ndani wakati ukweli ni kuwa hii ndio lebo bora zaidi Afrika,” alisema rapa huyo.

“Kama itatokea kuondoka hapa basi ni lazima niende kwenye lebo kubwa zaidi kama Young Money au Roc Nation,” aliongeza rapa huyo.


Lebo ya WCB iko chini ya Diamond Platnumz na imefanya kazi kubwa ya kuinua kipaji cha staa huyo ambaye hivi karibuni amevunja uhusiano wake na Jackline Wolper.

No comments