HARUNA NIYONZIMA AIPASIA YANGA KIUNGO FUNDI WA UKABAJI

KIUNGO Haruna Niyonzima ameipa dili klabu yake ya Yanga baada ya kuwapa jina la kiungo fundi wa ukabaji kutoka nchini kwao na tayari vigogo wa timu yake wameanza kulifanyia kazi.

Akiongea na saluti5, Niyonzima alisema katika mchezo wa wiki iliyopita kati ya Amavubi na Morocco, kiungo mkabaji wa taifa lake hilo alifanya kazi kubwa ambapo tayari ameshamshawishi kumleta Yanga.

Niyonzima alisema kinda huyo alianza kuonyesha kipaji chake muda mrefu katika nafasi ya ukabaji ambapo sasa ameridhika kwamba yuko tayari kuja Tanzania kuitumikia Yanga.

Niyonzima ambaye ni nahodha msaidizi wa Yanga, amesema kwamba endapo Yanga itafanya haraka kumnasa kiungo huyo itakuwa imeramba dume kama ambavyo ilivyofanya wakati alipompendekeza Thabani kamusoko asajiliwe kisha kuja kufanya kweli.

“Unajua sisi wachezaji tunajuana, sasa yule dogo nilikuwa namkubali muda mrefu lakini alikuwa bado hajakomaa ila kwa jinsi nilivyomuona mchezo wa juzi anafaa sana kuja Yanga,” alisema Niyonzima.


“Unajua Yanga bado tuna shida katika kiungo wa chini na ndio maana nikaamua kuwa jina hilo viongozi walifanyie kazi. Hii sio mara ya kwanza, utakumbuka nilishawahi kuwaambia wamsajili Kamusoko mapema na walipomsajili walimkubali.”

No comments