HIMID MAO ASEMA ATAPIMA OFA MPYA YA AZAM FC NA NYINGINE KUTOKA NJE YA NCHI

KIUNGO wa timu ya Azam, Himid Mao amesema kuwa ataweka kwenye mizani ofa mpya kutoka klabu yake ya sasa pamoja na zile atakazopata kutoka nje ya nchi.

Mao ameweka wazi kwamba anatarajia kumaliza mkataba wake na Azam mwezi Novemba, mwaka huu na bado hana uhakika ni wapi ataelekea.

“Mkataba wangu na Azam unaisha mwezi Novemba, ni suala rahisi tu kwa sababu nitalazimika kulinganisha ofa kutoka nje ya nchi na ile nitakayopewa na klabu yangu,” alisema kiungo huyo.

Azam imekuwa na wimbi la kukimbiwa na wachezaji wake muhimu tangu kuondoka kwa mshambuliaji wake mkongwe, John Bocco anayeripotiwa kusaini Simba.


Azam imeamua kubana matumizi yake kwa kutoa fedha ndogo za usajili na kuamua kuigeukia timu yao ya vijana ambao wana mpango wa kuwapandisha kuingia timu ya wakubwa.

No comments