HUSSEIN JUMBE KUTAMBULISHA WIMBO MPYA “UAMINIFU MTAJI” SIKU YA IDD MOSI


Mwimbaji asiyechuja katika miondoko ya dansi, Hussein Jumbe akiwa na bendi yake ya Talent, siku ya Idd Mosi atatambulisha wimbo wake mpya kabisa.

Wimbo huo unaokwenda kwa jina la “Uaminifu Mtaji” utatambulishwa ndani ya ukumbi wa Kisuma Bar, Temeke.

Hussein Jumbe ameiambia Saluti5 wimbo huo alioutunga yeye mwenyewe, ndio zawadi ya mashabiki wake kwa sikukuu hii ya Idd.


“Ni wimbo wenye ujumbe mzuri sana, upo kisasa na unakidhi soko la muda huu,” alisema Hussein Jumbe.

No comments