IBRAHIMOIVIC ASEMA ALIJUA MAPEMA KUWA SAFARI YAKE NA MAN U IMEFIKIA KIKOMO

MSHAMBULIAJI nyota raia wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic amesema kwamba alishaziona dalili zote kwamba hatakuwa katika kikosi cha Manchester United msimu ujao.

Manchester United imetangaza rasmi kuachana na na mshambuliaji huyo majeruhi ambaye anategeme kurejea tena dimbani mapema mwaka ujao.

Lakini hatimae United imeweka wazi kuwa hautamtumia tena mchezaji huyo na sasa iko sokoni kusaka mbadala wake.

“Wakati mwingine sisi binadamu tunatakiwa kusoma alama za nyakati,” amesema Zlatan juzi katika mahojiano na mtandao wa Shirika la habari Uingereza (BBC).

Zlatan mwenye miaka 35, alisaini mkataba wa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka 
mmoja zaidi.

No comments