IVAN PERISIC AIMBIA INTER MILAN IMWACHIE AJIUNGE NA MANCHESTER UNITED


WINGA nyota wa Inter Milan, Ivan Perisic ameiambia klabu yake kuwa anataka kujiunga na Manchester United kiangazi hiki baada ya kukubali ofa ya pauni 100,000 kwa wiki.

Kwa mujibu wa gazeti la Corriere dello Sport, Jose Mourinho alimtaja Perisic (28) kama kipaumbele katika usajili mapema msimu huu na alikuwa Croatia mwezi Machi kumalizana na kiungo huyo.

Kwa kukubali ofa ya United, Perisic atakuwa ameongeza mara mbili mshahara wake anaolipwa sasa na kilichobaki ni klabu hiyo ya Old Trafford kukubaliana dau na Inter Milan.

Klabu hiyo ya Serie A inaelezwa kutaka pauni milioni 53 imwachie nyota huyo, lakini United ina matumaini kuwa mazungumzo baina yao yanaweza kushusha kiwango hicho.

No comments