JAHAZI MODERN TAARAB KUTAMBULISHA NYIMBO MPYA EID EL FITR

MAGWIJI wa mipasho Bongo, Jahazio Modern Taarab wanatarajiwa kuzitumia shamrashamra za sikukuu ya Eid el Fitr kutambulisha ‘nondo’ zao mpya walizozisifu kwa kudai ni moto wa kuoteambali.

Jahazi Modern Taarab iliyo chini ya Prince Aboubakar Soud ‘Amigo’ siku ya Idd Mosi wanatarajiwa kumwaga burudani ndani ya ukumbi wao wa nyumbani wa Travertine Hotel, Magomeni, wakati Idd Pili watakuwa kwenye Dar Live, Mbagala, Dar es Salaam.

Mmoja wa mabosi wa Jahazi, Hamis Boha amesema kwamba Idd Tatatu watafunga pazia la shamrashamra za Eid el Fittr ndani ya Check Point, Kigogo Fresh, Chanika, ambako kote huko watawaonjesha mashabiki wao ladha ya nyimbo zao mpya.

“Tumekuwa kambini kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili sasa tukipika vibao vyetu vingine vipya ambavyo sasa tumepanga kuvitambulisha kwenye shoo zetu zote za Sikukuu ya Eid el Fitr,” amesema Boha.


Boha amesema Alhamisi baada ya Idd Tatu, tutakuwa Dar Safari Park, Buza, Ijumaa ndani ya Machokodo, Bagamoyo na Jumamosi Equator Grill, Mtoni kwa Azizi Ally, Dar es Salaam ambako kote huko mwendo utakuwa ni wa nyimbo mpya.

No comments