JAHAZI MODERN TAARAB WAANIKA RATIBA YA EID EL FITR

LIKIWA limesalia takriban juma moja tu kabla ya shamrashamra za sikukuu ya Eid el Fitr, tayari baadhi ya bendi za muziki zimeanza kuanika ratiba zao za shoo katika kipindi hicho.

Jahazi Modern Taarab chini ya mwimbaji Prince Aboubakar Soud ‘Amigo’ siku ya Idd Mosi wanatarajiwa kumwaga burudani ndani ya ukumbi wao wa nyumbani wa Travertine Hotel, Magomeni Sheli, jijini Dar es Salaam.

Bosi wa Jahazi Modern, Hamis Boha ameiambia saluti5 kuwa, Idd Pili watakuwa kwenye kiwanja cha maraha cha Dar Live, Mbagala Zakheem, jijini Dar es Salaam kabla ya Idd Tatatu kufunga pazia hilo ndani ya Check Point, Kigogo Fresh, Chanika.

“Alhamisi baada ya Idd Tatu, tutakuwa Dar Safari Park, Buza, Ijumaa ni ndani ya Machokodo, Bagamoyo na Jumamosi itakuwa pale Equator Grill, Mtoni kwa Azizi Ally, jijini Dar es Salaam,” amesema Boha.


Boha amewaomba mashabiki wao wote kuhudhuria kwa wingi kwenye shoo hizo zote, huku akiahidi mambo makubwa ikiwemo vibao vyao vipya ambavyo ni maandalizi ya albamu yao ijayo waliyopanga kuipakua hivi karibuni.

No comments